Image
Image

NEWS ALERT: Mradi wa barabara ya njia sita kutoka Dar es salaam kwenda chalinze (km 100) waiva.



Jopo la Wataalamu washauri katika mkutano uliokutanisha wadau mbalimbali ya sekta ya barabara nchini kujadili upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa ubia wa barabara  ya Dar - Chalinze.



Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa kujadili kuhusu upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa ubia wa barabara ya Dar - Chalinze uliofanyika jijini Dar es salaam.


Ramani ya barabara ya njia sita (tatu kila upande) ya Dar es Salaam - Chalinze – Morogoro.
Tayari maandalizi ya ule mpango wa kujenga barabara ya njia sita (tatu kila upande) Dar es Salaam – Chalinze-Morogoro (km 200) Express Way umeiva ambapo awamu ya kwanza itahusisha barabara ya Dar es Salaam (Biti Titi Jnct) – Chalinze (km 100) Express Way kwa utaratibu wa Public Private.
Barabara hiyo mbadala ambayo itakuwa ni ya kulipia itajengwa kwa njia sita (6 lanes).
Barabara iliyopo sasa itaendelea kutoa huduma kwa wale ambao hawako tayari kutumia barabara ya kulipia.
Habari njema ni kuwa, Wahandisi washauri wa michoro ya barabara hiyo tayari wameonyesha jinsi njia sita zitakavyojengwa. Kazi hii inategemewa kuanza mwaka huu, kwa mujibu wa wataalamu hao walipokuwa wakiwakilisha ripoti ya utafiti wa awali wa michoro ya barabara hiyo, New Afrika Hotel.
Barabara hii itajengwa kwa kwa utaratibu wa ubia kati ya serikali na makampuni binafsi (Public Private Partnership -PPP).


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment