Image
Image

Pesa za wizi za sambaa kama utitiri

WAZIRI wa zamani na Mkuu wa Usalama wa Taifa mstaafu, Dk. Hassy Kitine, amewataka Watanzania kutoacha kupokea fedha wanazohongwa na baadhi ya watu wanaosaka urais, kwa sababu zimeibwa kutoka kwao.
Katika mahojiano maalumu aliyoyafanya na Raia Mwema jijini Dar es Salaam wiki hii, Kitine alisema wananchi wanatakiwa kuzichukua fedha hizo lakini wachague viongozi wanaojua watawafaa pasipo kujali walichukua fedha za mafisadi.
“Kuna wagombea watawapa pesa. Kuleni hizo pesa. Msikatae. Pesa ni pesa. Aliyekuwa anazikataa labda Baba wa Taifa tu (Mwalimu Julius Nyerere).
“Kuleni, lakini kura yako ya kumchagua kiongozi wa kukuongoza haina thamani sawa na hizo pesa. Kura yako ni zaidi ya mamilioni ya fedha. Kura yako isilinganishwe na pesa.
“Hawa wagombea (baadhi) wanazo pesa ambazo ni za wizi. Wametuibia hapa. Wanayo mapesa mengi, kuleni pesa zao, lakini kura yako ni zaidi ya thamani ya pesa hizo.
“Pili, fika kwenye Mkutano Mkuu (CCM) halafu kituo cha kura baadaye mpigie mtu unayemuona ni mtu safi. Na usafi huo unatokana na uwezo wa kukataa rushwa.
“Kwa upande wangu nasema mimi sijajaza fomu. Lakini kama nisingekuwa mwadilifu, ningetaka kuwa na mapesa mengi, ningekuwa na mapesa hayo, mengi kuliko wote hawa wanaotaka urais.
“Ningekuwa nachota kule Usalama wa Taifa wakati niko mkubwa na kisha leo ningetoa rushwa. Lakini siwezi kuchanganya pesa na uongozi wa nchi,” alisema Kitine katika mahojiano ambayo yamechapwa ndani ya gazeti hili.
Katika mahojiano hayo ambayo Kitine ameongea kwa kirefu kuhusu historia ya maisha yake ya utumishi, alisema kama Watanzania watamuona anafaa kuwa Rais, yeye yuko tayari kuwatumikia.
Alisema anajua ana ufahamu mkubwa kuhusu Tanzania na watu wake pengine kuliko mwanasiasa yeyote ambaye ametajwa kutaka kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
“Kama Watanzania wanaona naweza sitaogopa. Lakini mimi sina pesa. Uongozi wa sasa ni pesa. Lakini naweza kuwa rais bora zaidi. Nitakuwa rais bora zaidi kama nikipewa nafasi.
“Katika watu waliojitokeza kutaka urais hakuna hata mmoja anayeifahamu hii nchi kuliko mimi. Naijua nchi hii, pia ni msomi niliyebobea nina digrii nne.
“Mimi ni mchumi. Naujua uchumi wa nchi. Najua usalama. Hakuna hata mmoja anayejua usalama kama mimi. “Hakuna mtu anayejua matatizo ya ulinzi kama mimi. Hakuna mtu anayejua usalama wa nchi kama mimi.
“Hatutaki mambo kama ya Tanga (ugaidi) lazima kuwe na wa kukemea. Simtishi mtu, nazungumza habari ya nchi. Sina cha kulipiza kisasi,” alisema.
Katika mahojiano hayo ya kusisimua, Kitine alieleza namna uamuzi wake wa kuagiza gari kutoka nje ya nchi ulivyomletea matatizo mbele ya Nyerere.

- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/pesa-za-wizi-zasambazwa#sthash.ZvW0rNM3.dpuf

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment