Image
Image

Ubalozi wa marekani watoa tahadhari ya shambulio la kigaidi nchini uganda


Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umetoa tahadhari ya dharura kwa raia wake nchini Uganda hapo jana inayosema kuwa kunauwezekano wa kuwepo kwa tishio la kigaidi Jijini Kampala.
Ubalozi wa Marekani umepata taarifa za kuwepo kwa uwezekano wa tukio la shambulizi la kigaidi eneo ambalo raia wa nchi za magharibi wakiwemo wa Marekani hupenda kukaa Jijini Kampala, na tukio hilo linaweza kufanyika mapema mno.
Ubalozi wa Marekani haujatoa taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo, lakini nchi ya Uganda ambayo ni rafiki na Marekani na yenye majeshi yake nchini Somalia ilishashambuliwa siku za nyuma na wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment