Raia wa UFARANSA NANE na marubani wawili raia wa ARGENTINA wamefariki dunia pale HELIKOPTA mbili zilipogongana kwenye jimbo la LA RIOJA kaskazini magharibi mwa ARGENTINA.

FLORENCE ARTHAUD, muogeleaji wa OLYMPIC CAMILE MUFFAT pamoja na bondia wa mashindano ya OLYMPIC ALEXIS VASTINE walithibitishwa kupoteza maisha na ofisi ya Rais wa UFARANSA FRANSWA HOLLANDE.
CAMILE MUFFAT alifanikiwa kunyakua medali TATU kwenye bwawa la kuogelea kwenye mashindano ya OLYMPIC mwaka 2012 mjini LONDON wakati ALEXIS VASTIE alifanikiwa kuchukua medali ya SHABA kwenye mchezo wa ngumi mjini BEIJING mwaka 2008.




0 comments:
Post a Comment