Image
Image

Wananchi manyara waombwa kushirikiana na jeshi la polisi ili kufichua mauaji ya vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto

Wakaazi wa mkoa wa MANYARA, wametakiwa kulisaidia jeshi la polisi mkoani humo kufichua vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto vilivyokithiri mkoani humo ili kukomesha vitendo hivyo vinavyokwenda kinyume na haki za binadamu.
Wito huo umetolewa mjini BABATI mkoani humo na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto, Naibu Kamishina wa Polisi -DCP ADOLFINA CHIALO, wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo maafisa na wakuu wa dawati la Jinsia na watoto kutoka jeshi la polisi mkoani Manyara
Mafunzo hayo yanafanyika huku Takwimu zilizotolewa miaka miwili iliyopita na Wizara ya Afya na Usatwi wa Jamii zikibainisha kuwa mkoa wa Manyara, umekuwa kinara wa matukio ya ukeketaji ambapo inadadiriwa kuwa asilimia 15 ya wanawake wa mkoa huo wamekeketwa huku kiwango cha ukatili wa namna hiyo kikifikia asilimia 71, na kufuatiwa na mikoa ya Dodoma, ARUSHA, SINGIDA, MOROGORO na TANGA ambavyo ukatili umefikia kati ya asilimia 20 hadi 64.
Kutokana na changamoto hizo Mtandao wa Kijinsia hapa nchini-TGNP kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulika na masuala ya idadi ya watu duniani, UNFPA na Shirika la GTI, wamefadhili na kuendesha mafunzo ya namna ya kushughulikia makosa ya unyanyasaji na ukatili huo wa Kijinsia.
Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) ADOLFINA CHIALO, amewata askari waliohudhuria mafunzo hayo kutunza siri za watu wanaokwenda kwenye madawati yao kulalamikia vitendo vya ukatili na unyanyasaji wanavyofanyiwa huku wananchi wakiombwa kutoa taarifa za matukio hayo.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa MANYARA, SSP CHRISTOPHER FUIME, amesema kuwa vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vya ukeketaji watoto wa kike havikubaliki
Wakati wa Mafunzo hayo, Mtandao wa Kijinsia hapa nchini TGNP na washirika wake wametoa msaada wa kompyuta tatu zitakazotumiwa na waratibu wa madawati ya jinsia na watoto kwenye vituo vya polisi katika wilaya za BABATI, KITETO na SIMANJIRO.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment