Image
Image

Watu watatu wafariki Dunia baada ya kuangukiwa na kifusi wakiwa katika shughuli za uchimbaji madini tarafa ya kwimba,wilaya ya chunya, Mkoa wa Mbeya.


Na.Msaka Noti
Wachimbaji watatu wadogo wa madini ya dhahabu wamekutwa wamekufa kwenye shimo la Urefu wa Futi 50 walikokuwa wakichimba dhahabu baada ya kuangukiwa na Kifusi katika kitongoji cha Mawowo, kijiji cha Patamela, kata ya saza,tarafa ya kwimba,wilaya ya chunya, Mkoa wa Mbeya.

Kwamujibu wa kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya  SACP- Ahmed Msangi amesema kuwa chanzo cha tukio hilo la kupoteza maisha kwa wachimbaji hao wadogo wa madini katika shimo hilo nikutokana na kuta za shimo hilo kulowa maji na hivyo kukosa uimara na kiasha kuporomoka na kusababisha vifo.


Aidha Kamanda Msangi amewataja waliopoteza Maisha baada ya kuwatambua kuwa ni wanaume ambao umri wao nikuanzia miaka 26 hadi 35 ambapo mmoja kati ya hao watatu ni Victor Sanga ni Mkazi wa Mbeya ila wawili walio baki hawakutambuliwa maramoja kuwa niwakazi wawapi na kwamba miili yao  imehifadhiwa kwenye hospitali ya Mwambani Chunya, Hivyo Upelelezi zaidi wa tukio hilo unaendelea.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 12.03.2015. 
·          WATU WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI WAKIWA KATIKA SHUGHULI ZA UCHIMBAJI MADINI. 
·          MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI JIJINI MBEYA. 
·          WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA KETE ZA BHANGI. 
·         KATIKA TUKIO LA KWANZA: 
·          WATU WATATU WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. VICTOR SANGA (26) MKAZI WA MBEYA 2. AMEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA SHETA UMRI KATI YA MIAKA 30-35 NA 3. HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI, JINSI YA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 30-35, WOTE WACHIMBAJI WADOGOWADOGO WA MADINI/DHAHABU  WALIKUTWA WAMEKUFA KWENYE SHIMO LENYE UREFU WA FUTI 50 WALIMOKUWA WAKICHIMBA DHAHABU BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI.
·          TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 11.03.2015 MAJIRA YA SAA 19:15 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MAWOWO, KIJIJI CHA PATAMELA, KATA YA SAZA, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO TUKIO HILO NI BAADA YA KUTA ZA SHIMO KULOA MAJI NA KUKOSA UIMARA NA KISHA KUPOROMOKA. 
·          MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MWAMBANI CHUNYA. UPELELEZI ZAIDI WA TUKIO HILI UNAENDELEA.
·         KATIKA TUKIO LA PILI: 
·          MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA STEWARD MANDRAS (55) MKAZI WA UYOLE ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LISILOFAHAMIKA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.
·          TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 11.03.2015 MAJIRA YA SAA 19:10 JIONI HUKO ENEO LA SIJABAJE-UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO, JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
·         TAARIFA ZA MISAKO:
·          WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. DIAMUND MANYERERE (24) MKAZI WA MOPOROMOKO NA 2. REMSI BUNGE (20) MKAZI WA MAKAMBINI WILAYANI MOMBA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI KETE 03 SAWA NA UZITO WA GRAM 15.
·          WATUHUMIWA WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 11.03.2015 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI HUKO KATIKA MSITU WA IDARA YA MAJI, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
·          KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WACHIMBAJI MADINI KUWA MAKINI HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA KWA KUCHUKUA TAHADHARI ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA ALIYESABABISHA KIFO NA KISHA KUKIMBIA AZITOE ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE. 
·         Imesainiwa na:
·         [AHMED Z. MSANGI – SACP]
·         KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment