Image
Image

Askari wengine wa Kiafrika wauawa nchini Somalia


Umoja wa Afrika (AU) umethibitisha kuwa askari wake watatu wameuliwa katika shambulizi ya kuvizia lililofanywa na kundi la al Shabab huko kusini mwa Somalia.
Mjumbe wa Umoja wa Afrika nchini Somalia Maman Sidikou amesema askari hao watatu walishambuliwa ghafla katika eneo la Lower Shabelle huko kusini mwa Somalia.
Hata hivyo msemaji wa kundi la al Shabab Abdulaziz Abu Musab amesema kundi hilo limeua askari 5 wa Umoja wa Afrika na kwamba wote walikuwa kutoka Burundi. Umoja wa Afrika haukueleza utambulisho wa askari hao.
Siku moja kabla ya mauaji hayo wapiganaji wa kundi la kigaidi la al Shabab pia walikuwa wameua askari watatu wa Kenya wanaohudumu katika kikosi cha majeshi ya Afrika yanayolinda amani nchini Somalia AMISOM na kujeruhi wengine 8.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment