Image
Image

Chama cha walimu Tanzania mkoani mara kimepinga agizo la mkuu wa mkoa la kuwataka kubadili ratiba za masomo.


Chama cha walimu Tanzania CWT mkoa wa mara wamepinga agizo la mkuu wa mkoa huo ambalo   liliwataka maafisa elimu wa wilaya zote na kubadili ratiba za masomo na kuweka utaratibu  utakawezesha  wanafunzi kusoma kuanzia saa moja na nusu hadi saa kumi na nusu jioni badala utaratibu awali wa muda wa  masomo kunza saa  moja  na  nusu hadi saa nane  mchana.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa CWT mkoa wa mara,mwenyekiti  wa  chama hicho mkoa Bw. Livingstone Gamba,amesema  agizo  hilo la mkuu wa mkoa kamwe haliwezi   kutatekelezwa kwa vile linalenga kuvuruga ratiba za vipindi vya masomo hasa wakati wa mchana  wakati walimu watapolazimika kwenda nyumbani kutafuta chakula cha mchana.

Hata hivyo mwenyekiti huyo wa CWT mkoa wa mara,amesema endapo serikali kupitia kwa mkuu wa mkoa  itataka agizo hilo litekelezwe lazima  wadau wote washirikishwe na kufanya maandalizi ya  kuwalipa posho za chakula kwa walimu ikiwa ni pamoja malipo ya muda wa ziada.

Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa mara  Kapt.Mstaafu Aseri Msangi,ametaka kufanyika kwa mabadiliko  hayo ya muda wa masomo  kwa lengo la kuinua taalum,kuwapa watoto muda wa mapumziko na kufufua michezo mashuleni.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment