Image
Image

Ikulu imekana kuwepo kwa njama zozote za kutaka kumdhuru mwenyekiti mtendaji wa IPP LIMITED, DK. REGINALD MENGI.


Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais,Ikulu, Salvatory  Rweyemamu.
Ikulu imekana kuwepo kwa njama zozote za kutaka kumdhuru mwenyekiti mtendaji wa IPP LIMITED, DK. REGINALD MENGI, zilizodaiwa kuandaliwa na Rais Jakaya Kikwete, kwa kile kilichodaiwa kuwashughulikia wanaoihujumu serikali yake na kupanga kumshughulikia baada kustaafu.
Habari hizo ziliripotiwa na gazeti la TAIFA IMARA ambazo zilikuwa na kichwa cha habari ZITTO AMCHONGEA MENGI KWA JK na kudai kunasa mazungumzo kati ya Rais Kikwete na kiongozi wa chama cha ACT-WAZALENDO, Zitto Kabwe ambaye kwa wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa PAC, ambaye inadaiwa alimchongea kwake kwamba, ndiye kinara anayesababisha serikali yake iyumbe kila mara.

Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais,Ikulu, Salvatory Rweyemamu, amewaeleza wandishi wa habari jijini dar es salaam kuwa Rais aliposikia habari hizo akiwa nje ya nchi alishtushwa nazo na kwamba Rais hawezi kushiriki njama za kumdhuru raia na kuongeza kuwa habari hizo ni za kutengenezwa kwa nia mbaya ya kuharibu uhusiano mzuri uliopo kati ya Rais na Dk. Mengi.

Akizungumzia suala la Rais kusaini au kutokusaini miswada mbalimbali iliyopitishwa na bunge ukiwemo wa takwimu na makosa ya mtandaoni ambazo baadhi ya wadau wa habari na tasisi mbalimbali zimekuwa zikimsihi Rais asisaini hadi zifanyiwe marekebisho Rweyemamu amesema Rais atasaini yote kwani ilipitia taratibu zote.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment