Image
Image

Yanga watwaa ubingwa, waishushia polisi kichapo kitakatifu cha goli 4 kwa moja uwanja wa taifa Dar es Salaam.


Yanga SC wamefanikiwa kuwavua ubingwa Azam FC hii leo, baada ya kuwashusha daraja Polisi Morogoro, baada ya leo kushinda goli 4-1, huku Amisi Tambwe akiwa mchezaji wa kwanza kufunga hatrik mbili katika msimu huu wa ligi kuu ya vodacom.
Katika mchezo wa leo yanga sc waliuwanza mchezo kwa kasi na katika dakika ya kwanza amanusura wapate goli kupitia kwa Amisi Tambwe, na katika dakika ya 8 kichwa cha Kpah Sherman kiliokolewa vyema na kipa wa Polisi Morogoro.


Baada ya dakika 10 za mchezo Polisi Morogoro walianza kuushika mchezo na kuanza kutawala, huku wakitengeneza nafasi mbili za kujipatia magoli, ambapo walizipoteza.
Katika dakika ya 41 kazi nzuri ya Saimun Msuva ilihitimishwa vyema na Amis ambwe ambapo aliandika goli la kwanza kwa yanga sc katika mchezo wa leo, na kupelekea kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.
Kipindi cha pili Polisi Morogoro walirejea kwa kasi huku yanga wakiweka mpira chini na kucheza soka la kuonana na la uhakika.
Alikuwa Msuva tena aliyetanguliziwa mpira na kupiga shuti lililopanguliwa na kipa wa Polisi Morogoro na mpira kumkuta, Amis Tambwe aliyeiandikia yanga goli la pili katika dakika ya 52.

Dakika 7 mbele Amisi Tambwe aliiandikia yanga goli la tatu, likiwa goli lake la 14 msimu huu wa ligi kuu ya vodacom na kuwa hat-trik ya pili msimu huu.
Saimon Msuva aliitimisha kalamu ya magoli kwa upande wa yanga katika dakika ya 66 baada ya kuvunja mtego wa kuotea na kufikisha magoli 17 katika msimu huu wa ligi kuu ya vodacom.
Poloisi Morogoro ambao walipoteza kujiamini na kupelekea kupoteza mipira ovyo toka kuingi kwa goli la tatu, waliandika goli la pekee katika dakika ya 83 kupitia kwa Bantu Admin na kupelekea mpira kumalizika kwa yanga kuibuka na ushindi wa goli 4-1.
Kwa matokeo hayo yanga wamefikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote, hivyo kutwaaza mabingwa wa bara wa msimu huu wa ligi kuu ya vodacom.
Ubingwa huu ni wa 25 kwa yanga toka ligi kuu ya Tanzania bara ianze, huku Simba SC wakitwaa ubingwa huo mara 18, wakifuatiwa na Mtibwa sugar mara 2, huku Azam FC, Pan Afrikan na Mseto wakitwaa mara moja.
Kwa matokeo ya leo ina waweka katika mazingira mabaya Polisi Morogoro ya kusalia katika ligi kuu ya vodacom ambapo wamebakisha mchezo mmoja wakikwa katika nafasi ya 13, wakiwa na pointi 25 sawa na Ndanda FC na T.Prisons waliobakiwa na michezo miwili.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment