Image
Image

Jumla ya vijiji 14 vya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe vinatarajia kuanza kunufaika na mpango wa umeme vijijini


Jumla ya vijiji 14 vya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe vinatarajia kuanza kunufaika na mpango wa umeme vijijini hadi ifikapo mwezi juni mwaka huu ambapo tayari kazi ya kusimika nguzo za umeme kwenye baadhi ya vijiji ukianzia kitongoji cha ngalawale wilayani humo umeshaanza.
Kazi kubwa inayoendelea hivi sasa kuhakikisha mradi huu wa umeme unawafikia wananchi vijijini ukitokea mjini ludewa ni kuchimba mashimo ya kusimika nguzo za umeme kazi ambayo inafanywa na wananchi kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo la ludewa,Mh. Deo filikunjombe pamoja na mkandarasi aliyepewa kazi hiyo.

Akishiriki kazi ya kuchimba mashimo na kusimika nguzo za umeme, Mh.Filikunjombe ambaye amebeba jukumu la kuhakikisha umeme unawafikia wananchi wake kwa wakati, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumuunga mkono katika kujiletea maendeleo badala ya kuishia kuwa walalamikaji. 

Bwana Godson Mshana ni mmoja wa wananchi wa ngalawale-ludewa aliyejitolea kufyeka mahindi katika shamba lake bila malipo kuunga mkono mradi huo wa umeme.

Awali akiongea na wananchi wa vijiji vya lifua, luilo, ngalawale na ngelenge,Mh.Filikunjombe amewatoa wasiwasi wananchi kuhusu gharama za kujiunga na huduma ya umeme huo pindi utakapokamilika na kwamba gharama zake zitakuwa shilingi 27,000 tu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment