Image
Image

Wakulima Arumeru wavamia duka la wakala wa mbegu baada ya kuuziwa mbegu feki.


Wakulima wa kata ya king'ori wilayani arumeru mkoani Arusha wamevamia Duka la wakala wa pembejeo lililoko katika kata hiyo wakitaka walipwe fidia ya hasara ya mamilion ya fedha baada  ya kununua mbegu zinazodaiwa kupita muda wa matumizi na wameiomba serikali kuwasaidia.
Wakizungumza kwa jazba huku wakionyesha moja ya shamba lililoteshwa mbegu hizo ambazo hazikuota  wakulima hao wamesema kwa sasa hawataki tena fidia ya mbegu bali wanataka fidia ya gharama  za  kilimo kwani hii nimara pili kupewa mbegu sizizoota na kwamba kama serikali haitachukua hatua  watachukua wao wenyewe .
Akizungumzia malalamiko hayo wakala huyo Bw. Melikizediki Nnko amesema alishapokea malalamiko  hayo na kuyafikisha kwenye kampuni husika na ikakubali kulipa fidia na hata yeye anashangaa  kuona kuwa hata mbegu walizofidiwa hazioti.
Afisa kilimo wa halmashauri ya meru Bi.Grace Solomon amesema malalamiko hayo pia yalishafika ofidinai kwake na wakalifikisha kwa wakaguzi  wa  mbegu  ambao pia  walithibitisha kuwa  zilikuwa hazina viwango na kampuni husika ikatakiwa kuwafidia wakulima hao mchakato ambao bado  unaendelea licha ya kukabiliwa na changamoto nyingi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment