Image
Image

Kituo cha Mafuta kujengwa karibu na Ardhi OEVU mto RUAHA kwenye eneo la NDIUKA - IPOGORO


Uongozi wa mkoa wa IRINGA umeridhia kujengwa kwa kituo cha mafuta kwenye eneo la NDIUKA - IPOGORO linalopakana na ardhi oevu ya Mto RUAHA mdogo katika Manispaa ya IRINGA baada ya kujiridhisha na taarifa ya Baraza la Taifa la Hifadhina Usimamizi wa Mazingira- NEMC.
Mkuu wa mkoa wa IRINGA - AMINA MASENZA amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho kinachojengwa na Kampuni ya PUMA umepata kibali baada ya NEMC kufanya tahmini ya athari za kimazingira na kutoa masharti ya kuzingatia wakati wa ujenzi.
Eneo la Ndiuka kando kando ya barabara Kuu ya Iringa –Dar Es Salaam ni upande wa pili wa inapopatikana ardhi oevu ya chanzo cha maji cha mto Ruaha, na hapo ndipo kitakapojengwa Kituo hicho.
Ujenzi wa Kituo hicho ulisimama mwishoni mwa 2014 baada ya kuwepo na malalamiko ya wananchi na wadau wa mazingira juu ya usalama wa uchafuzi wa chanzo cha maji na hivyo mkoa kuingilia kati na kuwakutanisha wadau wa pande zote kujiridhisha na usalama wa chanzo hicho kwa afya za wananchi.
Mkuu wa mkoa wa IRINGA, AMINA MASENZA amesema baada ya NEMC kurudia tena kufanya tathimini ya athari za mazingira wamejiridhisha kuwa eneo hilo halitaathiri chanzo hicho.
Kwa upande wake meneja wa Ufundi anayehusika na mafuta ya Petrol Kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji –EWURA- Mhandisi Gerald Maganga anasema kuwa vibali hutolewa baada ya mwekezaji kutimiza masharti yote ikiwa ni pamoja na taarifa ya NEC.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment