Image
Image

Siri ambayo itapunguza kutokuwepo kwa mimba za utotoni kwa vijana wa kike katika shule za msingi,Sekondari ya bainika.


Kuwepo kwa  sheria na sera katika shule za msingi,Sekondari na  kutoa elimu kwa wanajamii hasa wazazi na walezi kutapunguza mimba za utotoni zinazo sababisha vijana wa kike kushindwa  kuendelea na masomo,kupoteza maisha yao na watoto watakaowazaa.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Temeke ,   Mwalimu CHAVILA DONALD  alipokuwa   akifungua mafun zo ya elimu ya  afya ya uzazi,  jinsia  na stadi za maisha ,   kwa wanafunzi  na walimu wa shule za Sekondari za wilaya hiyo yaliyofanyika katika shule ya Sekondari Kibasila.

Mwalimu CHAVILA  amesema wanafunzi ni watu muhimu  wanategemewa katika familia, jamii na taifa katika kuleta maendeleo na kupunguza umaskini.

Kwa upande wa  walimu amewahimiza  kuwa msaada wa kitaaluma na kijamii kwa wanafunzi na kuhakikisha watoto wanapata elimu bora itakayowakwamua kifikra, kijamiii na kiuchumi.

Naye Meneja Uraghibishi  na Mawasiliano kutoka Taasisi ya Wanawake  na Maendeleo - WAMA-   PHILOMENA MARIJANI  ame sema mafunzo hayo ya siku tano yako chini ya mradi wa kuzuia mimba za utotoni katika shule za sekondari unaotelelezwa na Taasisi hiyo na Engender    Health kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la watu wa Marekani.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment