Image
Image

Mbunge NATSE awataka wananchi wa karatu kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.


Mbunge wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) ambaye pia Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini akiwa anateta jambo meza kuu.

Wananchi waliojitokeza kwa wingi wakiwa wanamsikiliza Mbunge wao akihutubia mkutano wa hadharakatika uwanja wa mazingira bora karatu mjini.

Mbunge wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse akiwa anasisitiza jambo jukwaani ambapo alisema njia bora ya kuwapiga chini chama cha mapinduzi CCM ni kwa kuhakikisha wananchi wanajiandikisha katika daftari la kudumu huku akidai safari hii ni jino kwa jino hadi ikulu.

Mwenyekiti wa vijana Wilaya ya Karatu John Male alisema lengo lao ni kuwaelimisha wananchi hata wasio wanachama kuhusu umuhimu wakujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Mbunge wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) ambaye pia Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini akihutubia wananchi wake katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa mazingira bora karatu mjini jana,amewataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu  la wapiga kura ambayo itawapa  fursa ya kuwachagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika ockoba mwaka huu. (Habari picha na Jamiiblog).
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment