Image
Image

Lukuvi amuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la mwanza kuwafikisha mahakamani watendaji wa ardhi wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya udanganyifu.


Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh.William Lukuvi amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la mwanza na manispaa ya ilemela kuwachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani baadhi ya watendaji wa ardhi katika halmashauri hizo wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya udanganyifu katika umilikaji na ugawaji wa ardhi na kusababisha malalamiko 395 ya migogoro ya ardhi.
Waziri Lukuvi ametoa agizo hilo jijini mwanza wakati akipokea taarifa ya malalamiko kutoka katika timu ya wataalam aliyoiunda mwezi mmoja uliopita ambapo amesema baada ya uchambuzi wa kina kufanyika imebainika kuwa malalamiko 141 kati ya 395 yanahusu fidia,70 yanahusu usimamizi duni wa kupanga, kupima na ugawaji wa ardhi, wakati malalamiko 54 yanahusu uelewa mdogo wa kanuni, sheria na taratibu kwa watendaji wa ardhi na wananchi na malalamiko 42 yanahusu uvamizi wa maeneo ya watu binafsi na ya umma hasa kwenye vilima.
Mh. Lukuvi amesema kwamba kwa wananchi ambao hawataridhika kabisa na hatua za serikali katika kushughulikia malalamiko yao amewaelekeza cha kufanya.
Kuhusu baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa katika manispaa ya ilemela na jiji la mwanza kujichukulia sheria mkononi na kuanza kugawa viwanja kwa wananchi - waziri huyo mwenye dhamana ya ardhi amesema ni kosa kisheria na bila kutafuna maneno kibao kikamgeukia mkurugenzi wa manispaa ya ilemela kwa kuvamia kiwanja cha mkazi wa bwiru alichokuwa amepewa na idara ya ardhi ya manispaa hiyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment