Image
Image

Ubovu wa Barabara wasababisha adha kubwa ya usafiri na hivyo mkuu wa mkoa kukwama kwa saa kadhaa Tunduru-SONGEA.


Mamia ya abiria wanaosafiri kwenda TUNDURU-SONGEA wamekwama njiani  kwa masaa  kumi   baada ya lori kukwama njiani kutokana na ubovu wa barabara uliotokana na mvua kubwa  zilizonyesha siku  mbili mfululizo wilayani tunduru.
Kutokana na ubovu huo wa bara bara mkuu wa wilaya ya tunduru  Bw. Chande Bakary  Nalicho   ambaye  pia alikwama njiani ameweza kukwama kwa saa kadhaa ambapo amesema kuwa hali hiyo imejitokeza kutokana na mvua   kunyesha na kuharibu  miundombinu ya Barabara .

Kwa upande wa msimamizi wa mradi wa matengenezo ya barabaraya NAMTUMBO-TUNDURU  Bw. Steven Byabato baada ya kuulizwa amekiri kuwempo khuko kwa ukiritimba wa miundombinu ila akasema kuwa   kinachofanyika sasa ni kuweza kuhakikisha  kwamba njia inapitika kwa urahisi hasa katika kipindi hiki cha matangenezo.

Hata hivyo wakandarasi wa kichina wanaotengeneza  barabara hiyo waliliondoa kwa kijiko au Staveta  Lori lililokwama eneo la  masonya baada ya mkuu wa wilaya naye kukwama eneo hilo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment