Image
Image

Mwenyekiti wa IPP DK.MENGI ametangaza zawadi ya Shilingi Milioni 50 kwa mtu atakaye toa taarifa za watu waliowaua wafanyakazi wawili wa kampuni ya Bonite Bottlers Moshi Jumatatu wiki hii.


Mwenyekiti Mtandaji  wa IP P, Dakta REGINALD MENGI ametangaza zawadi ya Shilingi Milioni 50  atakayetoa taarifa itakayowezesha kukamatwa, kush i takiwa ,   watu waliowaua wafanyakazi wawili wa kampuni ya  Bonite Bottlers Moshi  Jumatatu wiki hii.
Wafanyakazi   hao  wawili wa Bonite Bottlers Moshi , ambayo ni moja ya kampuni za IPP, wakiwa kwenye gari Toyota Hiace ,lenye namba za usajili T 803 ATR , waliuawa na watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi karibu na Kili FM Radio,barabara mpya ya Soweto mjini Moshi mkoa wa Kilimanjaro.

Watu hao walikuwa wamepanda pikipiki mbili mojawapo ikiwa ni aina ya Boxer.

Mauaji hayo ya kinyama yaliyoondoa roho za wafanyakazi  hao  waliokuwa wakitegemewa na kampuni na familia zao yanasikitisha sana na  Mwenyezi  Mungu azilaze roho za marehemu  hao  mahali pema peponi.

Wakati uchunguzi wa mauaji hayo unafanywa na Polisi, mtu ye   yote mwenye taarifa zozote kuhusu uhalifu hu o  atoe taarifa kituo chochote cha Polisi hapa nchini.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment