Image
Image

News Alert:Mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida,imewahukumu madereva wanne wa magari ya abiria na mizigo, adhabu ya kutumikia jela jumla ya miezi kumina mbili


Mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida,imewahukumu madereva wanne wa  magari ya abiria na mizigo, adhabu ya kutumikia jela jumla ya miezi kumina mbili  na kulipa faini ya jumla ya shilingi elfu themanini  baada ya kupatikana na hatia ya kukiuka sheria za  usalama barabarani ikiwemo ya kuendesha magari yakiwa mabovu,kuegesha maeneo yasi ruhusiwa na kujaza abira wengi kupita kiasi  jambo ambalo  linahatarisha maisha ya  abiria..
 Mwendesha mashitaka  na mwanasheria wa serikali,Pridence Mutta,alidai mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo,Joyce Minde kuwa mnamo aprili 20 mwaka huu majira ya asubuhi huko katika kata ya Ipembe mjini hapa,dereva Willson John miaka ishirini na tatu  mkazi wa kititimo manispaa ya singida,alikamatwa akiwa amepakia abiria wengi kwenye lori dogo aina ya fuso  lenye usajili wa namba T.354 BGX  kinyume na Sheria.
Naye dereva wa FUSO T.674 ERM  Simon David  miaka thelathini na Saba mkazi wa moshi mjini mkoani kilimanjaro,amepatikana na hatia ya kuendesha gari na magurudumu yake yakiwa yamechaa na kiti cha dereva kibovu hakifai,pia mshitakiwa wa mwisho Bwana Juma Ramadhani  miaka ishirini na mbili mkazi wa mtinko jimbo la Singida kaskazini,amehukumiwa kwenda jela miezi mitatu baada ya kukutwa akiendesha gari likiwa katika hali mbaya.
Kabla ya kutolewa kwa adhabu,mwendesha mashitaka Mutta aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa washitakiwa itakayokuwa fundisho kwake na madereva wengine ambao hawatii sheria za usalma barabarani na kuhatarisha maisha ya wananchi.
Hakimu Minde,alisema ili kuondoa dhana iliyoota mizizi kwa baadhi ya madereva kwamba makosa ya usalama barabarani, adhabu yake ni kulipa faini tu na mshitakiwa anao uwezo wa kulipa na kuachiwa huru, kwa hiyo washitakiwa wote wanne kila moja amepewa  adhabu ya kwenda jela miezi mitatu na akimaliza adhabu ,atalipa faini ya shilingi  elfu ishirini  ndipo urudi nyumbani kwake.
Aidha hakimu  Ninde  amesema kwa sasa hali ni mbaya kila siku ni ajali  ambazo  zinazopoteza nguvu kazi na kuziacha familia bila kuwa na wategemezi,hii yote inasababishwa na madereva kutokutii sheria za usalama barabarani na wakati mwingine  mahakama nazo kutokutimiza wajibu wake ipasavyo kwa kutoa adhabu ya  faini badala ya kifungo pamoja na  faini. 
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani  mrakibu msaidizi wa polisi ASP JOSEPH BUKOMBE  amesema  wameamua kuchukuwa jukumu la kuwapeleka mahakamani na bila ya kuwatoza faini kwa sababu makosa yao yamekuwa yaki jirudia kila wanapo kamatwa. 
Katika hatua nyingine ASP BUKOMBE  amesema wamekamata pikipiki na bajaji zaidi ya thelathini na tano   zilizo kuwa na makosa kwa lengo la kuwataka waajiri wa pikipiki hizo kufika kituoni ili washitakiwe wao na madereva wao ambao wengi wao  wamekuwa wakiendesha  bila leseni,kuvunja sheria za barabarani nakusababisha ajali ambazo zina garimu maisha ya  abiria bila sababu.  
Kwaupande wao  baadhi ya madereva walio fika mahakamani kwa ajili ya kujaribu kuwawekea dhamana wenzao  na zoezi hilo kugonga mwamba wamesema kuwa barabara zote katikati ya manispaa ya Singida hakuna sehemu ambayo kuna kibao cha kuegesha gari  , kwahiyo wameiomba manispaa ya Singida  kuweka vibao na kutenga maeneo ya maegesho,kwani kwasasa wamekuwa wakikamatwa  wanapo egesha magari na askari wa usalama Barabarani.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment