Image
Image

Rais Kikwete awaongoza watanzania Kuadhimisha miaka 51 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar viwanja vya Uhuru Dar es Salaam.


Rais  Jakaya Kikwete amewaongoza watanzania katika  kuadhimisha dhimisha miaka 51 wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar  uliounda  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaamna  kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta  JAKAYA KIKWETE sambamba na viongozi wengine wa serikali ya jamhuri ya muunganio na Zanzibar Katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Baada ya kuwasili uwanjani hapo akiwa  kwenye gari la wazi akiwa pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali DAVIS MWAMUNYANGE, Rais  KIKWETE alipokea  heshima  kutoka vikosi vya ulinzi na usalama na alipigiwa mizinga 21 na kisha kukagua gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama.
Wengine waliohudhuria sherehe hizo  za maadhimisho hayo ni pamoja na  Makamu wa Rais  Dakta MOHAMMED  GHARIB  BILAL,  Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza  la Mapinduzi, Dakta  ALI MOHAMMED SHEINna  Waziri Mkuu  MIZENGO PINDA.
Wengine ni Rais mstaafu BENJAMIN MKAPA, AMANI ABEID KARUME na  viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa, mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na wananchi.
Rais JAKAYA KIKWETE ambaye pia ni Amirijeshi Mkuu anashiriki maadhimisho hayo kwa mara ya mwisho katika nyadhifa hizo baada ya muhula wake unatarajiwa kwisha baadaeye mwaka huu baada ya uchaguzi mkuu unaorajaiwa kufanyika Oktoba.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment