Image
Image

Utafiti: Vyombo vya habari viripoti habari za Rushwa kuliko kuegemea zaidi kwenye habari za kijamii.


Utafiti  umeonesha  kuwa  asilimia  65  ya  watanzania   wanataka  vyombo  vya  habari viongeze nguvu  katika  kuripoti   masuala  ya  Rushwa  na   kuwafichua   viongozi  ambao  siyo  waadilifu  ambapo  kama  vyombo vya  habari  havitafanya   hivyo   ni   wazi kuwa  taifa  litaangamia.
Akiwasilisha  matokeo  ya  utafiti  huo  Bi. Rose Aiko  amesema,lengo  la  utafiti  huo ulikuwa  kuangalia  wananchi  wana mtizamo  gani  kuhusu  vyombo  vya  habari nchini,ambapo baadhi yao  wakionyesha  kutofurahia vyombo vya habari  kuripoti matukio mabaya kama ya   ajali za kutisha.
Baadhi  ya  watu  walioshiriki  katika  mkutano huo, akiwemo  wahariri  na viongozi  wa vyama  vya   siasa,wamekuwa  na  maoni  tofauti  kuhusu  utafiti  huo,huku wengine  wakisema  kuwa,vyombo vya habari  viongozewe  uhuru  ili  kuweza  kutoa taarifa  kwa  undani  zaidi  na  siyo  kutunga  sheria  ya kuvikandamiza.
Kwa  upande  wake  mkurugenzi  wa  utafiti   katika  uchumi  na maendeleo  wa  Repoa  Dkt. Donald   Mmari  amesema,tafiti  nyingi  wanazozifanya  zimeisaidia  jamii  kuongeza  umakini  na  kujenga uwezo wa kuhoji  mambo  mbalimbali  ya maendeleo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment