Image
Image

Mwanaume mmoja amuua mama yake Mzazi kwa kumchinja hadi kufa mkoani Singida.


Jeshi la polisi mkoani Singida, linamshikilia kijana Jumanne Yusuph miaka thelasini na tatu mkazi wa kijiji cha mtamaa‘a’,katika manispaa ya singida,kwa tuhuma ya kuhusika na mauaji ya mama yake mzazi.
Kamanda wa  polisi mkoani Singida, Thobias Sedoyeka, amesema kuwa,tukio hilo lilitokea jana, saa 12 alfajiri, huko katika kijiji cha mtamaa ‘a’, huku akimtaja marehemu huyo aliyejulikana kwa jina la Tausi Abdalah Miaka Hamsini na Sita, na kueleza kuwa siku ya tukio, kijana huyo alikwenda nyumbani kwa marehemu saa kuminambili alfajiri, kisha akamchinja au kumkata shingoni mama yake, ambaye alipoteza uhai papo hapo.
Akifafanua zaidi juu ya tukio hilo,Sedoyeka amesema kuwa,aprili 16 Mwaka huu, mtuhumiwa alifika kwa mama yake na kubomoa sahemu ya nyumba yake, kabla ya kumkamata mbwa na hatimaye kumchinja, kisha akatokomea zake kusikojulikana.
Kamanda Sedoyeka amesema kuwa,kutokana na historia ya mtuhumiwa kufanya fujo mara kwa mara, ndugu walimkamata na kumpeleka Hospitali ya mkoa wa Singida, lakini baada ya uchunguzi alirejea nyumbani na kutokana na marehemu  kuwa na hofu, ilibidi akalale kwa majirani na siku iliyofuata,majira ya alfajiri alirejea nyumbani kwake, kwa ajili ya kumjulia hali kijana huyo, na hapo ndipo alipokamatwa na kuuawa kwa kuchinjwa.
Kamanda Sedoyeka akielezea zaidi amesema kijana huyo  baada ya kumuuwa mama yake alikwenda kwa mama yake mkubwa kutoa tarifa, kisha tena akaenda kwa mwenyekiti wa kijiji kumjulisha kuwa, amefanya mauaji ya mama yake,na kabla ya mauaji hayo siku za nyuma mtuhumiwa alifanya tukio la kuwaua ng’ombe watatu wa mama yake kwa kuwacharanga na panga, wakati wakiwa machungani. 
Hata hivyo, Sedoyeka amesema kuwa, tayari wanamshikilia kijana huyo, kwa ajili ya uchunguzi zaidi, ikiwemo kumpeleka hospitalini, ili kupimwa akili zake,kutokana na tukio hili, sedoyeka amewataka wananchi wa mkoa wa singida na taifa kwa ujumla, kuchukua tahadhari, dhidi ya ndugu na jamaa, wanaoonekana kuwa na matatizo mbalimbali, ikiwemo maradhi ya akili.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment