Meneja
wa Tanesco mkoa wa Arusha Bw.Jenesisi
Kakore amesema hujuma hizo zilizofanywa
usiku zimesababisha sehemu kubwa ya nyaya zilizokuwa na moto kuanguka
chini jambo ambalo ni hatari kubwa kwa
maisha ya watu na viumbe wengine.
Aidha
Bw.Kakore amewata wananchi kuona umhimu wa kulinda miundombinu ya umeme na kutokubali kufumbia macho uharibifu kama huo
kwani watu hao licha ya kuwacheleweshea
kufikiwa na huduma wanachezea kodi zao.
Viongozi
na wananchi wa vijiji vya kata ya
orkokola ilikofanyika hujuma hiyo
wamesema huenda iefanywa na watu
wenye chuki ambao maeneo yao bado
hayafikiwa na huduma hiyo.
Hata
hivyo Bw. Kakore amewaomba wananchi wenye malalamiko na kero mbalimbali kuzifikisha ofisini kwake na kuachana na
dhana potofu ya kufanya hujuma kwani licha ya
kuwa kinyume cha sheria sio
suluhisho la tatizo.
0 comments:
Post a Comment