Image
Image

Chama cha ACT kimeitaka serikali kuwabana wamiliki wa mabasi kuweza kutoa mikataba ya kazi kwa madereva wao ili kuweza kudhibiti ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikitokea kila uchao.


Chama cha ACT kimeitaka serikali kuwabana wamiliki wa mabasi kuweza kutoa mikataba ya kazi kwa madereva wao ili kuweza kudhibiti ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikitokea kila uchao.
Kiongozi mkuu wa chama cha ACT wazalendo ndugu Zitto Zuberi Kabwe ameitaka serekali kuhakikisha inawabana wamiliki wa mabasi kote nchini  ili kuweza kutoa mikataba ya kazi   kwa madereva wao ili waweze kujulikana, kwa kufanya hivyo kuta punguza ajali ambazo siyo za msingi.
Kauli hiyo ameito wakati alipokuwa akiwahutubia mamia ya wakazi wa manispaa ya Singida na viunga vyake  kwenye mkutano wa kunadi chama cha ACT.

Kiongozi mkuu wa chama hicho Bwana. Zitto Kabwe ,amesema kuwa  aliyekuwa waziri wa uchukuzi Dk Harsson Mwakyembe aliunda tume ya uchunguzi wa ajali na mpaka sasa majibu hayaja tolewa jambo ambalo limekuwa likisababisha ajali kuendelea kutokea na kwa kipindi cha mwenzi Mach na April mwaka huu zaidi wa watu mianane wamesha poteza maisha kutokana na ajali za barabarani.
Ndugu Zitto amesema kuwa ilikupunguza ajali hizi za barabarani ambazo zimekuwa zikitokea kila uchao na kugharimu maisha ya watanzania wasio na hatia na kuwaacha na ulemavu na wengine kupoteza maisha chama hicho cha ACT kimeitaka serikali kutoa taarifa ya tume ya uchunguzi wa ajali  za barabarani zilizo fanyiwa utafiti ili kuweza kutafuta namna yakutatua matatizo ya ajali za mara kwa mara zinazotokea nchini.
Kwaupande mwingine mwenye kiti wa chama cha ACT Bi. Anna Mghwira na kada wa chama hicho Bwana  Selemani Msindi maarufu kwa jina la (Afande Sele) wamesema huduma nyingi  hasa za afya wakati wa zamani zilikuwa zikipatikana kulingana na uwezo wa serikali wakati ule, na kwasasa nchi imekuwa na utajiri mwingi wa madini ,kilimo na biashara,lakini cha kushangaza fursa hizo zimekuwa zikitumiwa na baadhi ya watu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment