Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kati Kati akishindikizwa na Naibu Waziri wa Mifugo
na Uvuvi Mh. Said Mohd Dimwa Kulia yake mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa
pamoja kati ya Uongozi wa Kampuni inayohusika na masuala ya Teknolojia ya
Kisasa ya mawasiliano ya Baharini { SRT } na watendaji wa sekta ya
Habarini hapo Zanzibar Ocean View.
Wa Pili kutoka Kulia waliokaa ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Kulia ya Balozi ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Said Mohd Dimwa na wa kwanza kulia ni Bwana Lazaria Moh’d Said.
Balozi Seif akizungumza na
Wanahabari mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa pamoja kati ya
Uongozi wa Kampuni inayohusika na masuala ya Teknolojia ya Kisasa ya
mawasiliano ya Baharini { SRT } ya Nchini Uingereza na watendaji wa
Taasisi zinazohusika na sekta hiyo hapo Zanzibar.
Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar ikiwa ni sehemu ya
Dunia hii inahitaji kuendelea kuwa salama na tulivu kutokana na mazingira
yake yaliyozunguukwa na Bahari pembe zote.
Alisema mfumo
wa kisasa wa mawasiliano unaotumika katika mataifa mbali mbali Duniani
uliolenga zaidi katika maeneo ya bahari yenye kutoa utajiri mkubwa kwa
asilimia 90% ya Uchumi wa Dunia unafaa kutumika ili kuondoa shaka
katika udhibiti wa uvamizi wa vitendo vya kiharamia.
Balozi Seif Ali
Iddi alisema hayo wakati akizungumza na Wanahabari wa Vyombo mbali mbali hapa
Nchini mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa pamoja kati ya Uongozi wa Kampuni inayohusika
na masuala ya Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini { SRT } ya
Nchini Uingereza na watendaji wa Taasisi zinazohusika na sekta hiyo hapo
Zanzibar Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
Alisema yapo
matukio kadhaa ya uvamizi wa vyombo vya Baharini yaliyowahi kuibuka na
kuripotiwa katika ukanda wa Pembe ya Afrika ambayo yalikuwa yakitekelezwa na
maharamia kutokana na udhaifu wa mawasiliano uliokuwepo wakati huo.
Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar aliridhika na kukubaliana na Mfumo wa kisasa waTeknolojia
ya mawasiliano ya Baharini unaotumiwa na Kampuni
ya { SRT } ya Nchini
Uingereza katika Mataifa mbali mbali Duniani ambao umesaidia kupunguza wimbi la
uharamia katika maeneo ya Baharini.
Akiwasilisha
mada ya mfumo wa utendaji kazi wa Kampuni hiyo kwenye Mkutano huo Afisa
Mkuu wa Mradi wa Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini wa { SRT
} Bwana Simon Tucker alisema kifaa maalum cha Mawasiliano huwekwa
kwenye chombo cha Baharini ambacho husaidia kutoa taarifa za mawasiliano.
Bw. Simon
alisema chombo hicho kidogo kinachoweza kuwekwa kwenye boti au hata meli za
uvuvi na abiria kinauwezo wa kusafirisha mawimbi ya mawasiliano kwa zidi ya
meli 40.
Othman Khamis
Ame
Ofisi ya Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment