Image
Image

David Cameron amemtaka Blatter ajiuzulu.


Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amemtaka Blatter ajiuzulu.
Hata hivyo rais wa Urusi Vladimir Putin amemuunga mkono bwana Blatter akisema bila shaka hizo ni njama za Marekani za kumtaka Blatter asiwanie tena uongozi wa FIFA.
Wakati huohuo Mmoja ya wafadhili wakuu wa kombe la dunia anasema kuwa huenda akalazimika kutathmini upya ufadhili wake kwa FIFA ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa kurejesha hadhi ya mchezo wa kandanda.
Taarifa kutoka kwa kampuni ya VISA inatolewa kufuatia visa vya kukamatwa kwa maafisa 7 wa vyeo vya juu wa FIFA kwa madai ya ulaji rushwa.
Wafadhili wengine nao wametoa maoni yao.
Kampuni ya Coca-Cola ilisema kuwa madai hayo yamechafua hadhi ya kombe la dunia huku kampuni ya magari ya Hyundai ikisema ina wasiwasi wa kesi zinazowaandama maafisa wa FIFA.
Blatter anawania muhula wake wa tano kama rais wa FIFA katika uchaguzi ulioratibiwa kufanyika hapo kesho
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment