Image
Image

Mbwembwe za Kaseke zamtokea puani Yanga.


MCHEZAJI mpya wa Yanga, Deus Kaseke, alitambulishwa kwa mbwembwe jijini Dar es Salaam mapema wiki hii na kuchimba mkwara, lakini kikubwa zaidi akanyoosha juu jezi namba nne ambayo ndiyo atakuwa anavaa.
Wakati huo mwenye jezi hiyo ambaye ni Rajab Zahir alikuwa sehemu anamchabo tu kiaina, baadaye akaibuka bwana.
 Rajab amelianzisha baada ya kuwaambia mabosi wake waliotoa jezi namba 4 na kumpa Kaseke kuwa wamechemsha kwani hiyo ni namba yake na hatakubali kunyang’anywa kirahisi.
Zahir alisema, hakubaliani na kitendo hicho na kwamba jezi namba nne ataitumia yeye kwa sababu ni mchezaji halali wa klabu hiyo na bado ana mkataba wa mwaka mmoja, Kaseke wamtafutie nyingine.
Akizungumza na Mwanaspoti, Zahir alisema: “Hata kama Kaseke ametambulishwa kuwa atavaa jezi namba nne, nitakayevaa ni mimi, yeye wamtafutie nyingine. Mimi bado mchezaji halali wa Yanga na nina mkataba wa mwaka mmoja mbele, hivyo mengine yanayoendelea siyajui, lakini kuhusu jezi, Kaseke wamtafutie nyingine.”
Mwanzoni mwa wiki hii, Yanga ilimsainisha Kaseke na kumtambulisha kwa mashabiki wake kuwa atatumia jezi namba 4 msimu ujao kama aliyokuwa anaitumia alipokuwa Mbeya City.
Awali, uongozi wa Yanga kupitia kwa msemaji wake, Jerry Muro, ulisema  umempa Kaseke jezi namba hiyo kwa sababu mkataba wa Zahir umemalizika na klabu iko kwenye mazungumzo na mchezaji huyo kwa ajili ya makubaliano ya msimu ujao.
Habari za ndani zinadai kwamba Yanga wanafikiria kumwacha au kumtoa kwa mkopo Rajab ingawa bado hawajataka kuiweka wazi.
Kaseke amtisha Msuva
Kaseke amemshtua mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara, Simon Msuva, anayemkuta klabuni hapo na kumwambia kwamba hamwogopi hata kidogo na kwamba atakomaa mpaka kieleweke.
Kaseke ambaye alisaini Yanga huku akiwindwa na Simba, alisema hali hiyo haitamvimbisha kichwa na kwamba Yanga inasifika kuwa na viungo wengi, lakini hatishiki na atapambana hadi kitaeleweka na akasisitiza Yanga itamfanya awe bora zaidi kikubwa apate ushirikino.
Kaseke aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja akitokea Mbeya City, alisema atakula sahani moja kwa kupambana na wakali kama Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Geofrey Mwashiuya, Salum Telela, Hassan Dilunga na wengine watakaosajiliwa mpaka kieleweke.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment