Image
Image

Namibia yafuzu robo fainali michuano ya COSAFA.


Timu ya taifa ya soka ya Namibia imefuzu katika hatua ya robo fainali katika michuano ya kutafuta taji la COSAFA.
Namibia ilifuzu katika kundi A baada ya kumaliza kundi hilo kwa wingi wa alama saba na kupata ushindi muhimu jana usiku baada ya kuishinda Zimbabwe mabao 4 kwa 1.
Katika mchuano mwingine, Mauritius iliwashinda Ushelisheli bao 1 kwa 0.
Namibia sasa itamenyana na Zambia katika hatau hiyo ya robo fainali juma lijalo.
Leo ni michuano ya kumaliza kundi la B, na mchuano muhimu leo ni katia ya Madagascar na Swaziland kwa sababu ni timu moja tu ndio inayostahili kufuzu.
Timu hizo zote zina alama 6.
Atakayefuzu atacheza na Ghana katika hatua ya nusu fainali.
Mchuano mwingine ni kati ya Tanzania na Lesotho zote ambazo zimeondolewa katika michuano hiyo kwa matokeo mabaya.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment