Viongozi na watumishi wa
Serikali wametakiwa kuwasaidia wakulima nchini ili wafikie
malengo ya kuzalisha chakula pamoja na mazao ya biashara kwa lengo la
kusaidia ukuaji wa sekta hiyo na pato la wakulima waliojiajiri katika sekta
hiyo inayotajwa kuajiri zaidi ya asilimia sabini ya wananchi wote .
Rai hiyo imetolewa Mjini
Iringa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe , Dakta REHEMA NCHIMBI alipokuwa
akifungua kikao cha viongozi wa Serikali,Maafisa Kilimo pamoja na
wafanyabiashara waliowekeza kwenye viwanda vya usindikaji mazao ya kilimo
pamoja na maziwa .
Amsesema iwapo Serikali itawasimamia vizuri wakulima na kuhakikisha
wanapata pembejeo na masoko ya mazao yao kilimo , kuna uwezekano wa kubadili maisha ya wakulima wadogo na
kuwaondoa kwenye umaskini wa kipato .
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
SAGCOT Centre ,Bwana GEOFREY KIRENGA amesema SAGCOT imekuwa kiunganishi kati ya
wakulima,Serikali na taasisi zinazo ji shughuli sh a na biashara ya mazao ya
kilimo pamoja na pembejeo kwa lengo la kuinua sekta ya kilimo na wakulima
wenyewe .
0 comments:
Post a Comment