Wanafunzi wa Darasa la Tatu
na la Nne katika Shule ya Msingi Msekela katika Kata ya Kalola Wilayani Uyui
Mkoani Tabora, wanasomea nje chini ya miti kwa zaidi ya miaka mitano .
Hali hiyo inadaiwa
inatokana na kile kinachodaiwa kuwa wananchi kukosa
mwamko wa kuchangia ujenzi wa madarasa .
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,Bwana LUCUS MPENA
amesema wanafunzi wameanza kusoma
wakiwa wanakaa chini tangu shule hiyo
ilipoanzishwa, mwaka 2009 na juhudi za
wananchi zimekuwa kidogo ambapo wa mefanikiwa kujenga madarasa mawili.
Mwanzilishi wa shule hiyo ya
Msekela,Bwana SHABANI KAYUGU
amesema shule hiyo iliyoanzishwa
ikiwa na wanafunzi wanafunzi 30 wavulana 13 wasichana 17 na sasa ina wanafuzi
320, ikiwa na darasa la awali lenye wanafunzi 35, ambao pia h usoma wakiwa chini ya miti.
0 comments:
Post a Comment