Image
Image

News Alert:Wakimbizi waliomba hifadhi kutoka nchini Burundi kufanyiwa uchunguzi na SERIKALI ya Tanzania.


Waziri wa mambo ya ndani ya nchi mh Mathias Chikawe amesema serikali itawafanyia uchunguzi waomba hifadhi wote waliokimbilia nchini kutoka nchini burundi na wale watakaobainika kutokuwa na sababu za msingi au nia ovu za kukimbia watachaukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kurudishwa burundi.
Waziri Chikawe ameeleza hayo baada ya kupokea taarifa ya ujio wa wakimbizi na kutembelea kambi ya muda katika uwanja wa lake tanganyika mjini kigoma, ambapo amesema serikali inafuatilia kwa karibu changamoto zilizojitokeza kufuatia ujio wa wakimbizi, ambapo katibu tawala wa mkoa wa kigoma mhandisi John Ndunguru ameeleza kuwa kijiji cha kagunga sasa kiko huru baada ya wakimbizi wote kusafirishwa lakini kinakabiliwa na tatizo la njaa, uharibifu wa mazingira, ugonjwa wa kipindupindu na uharibifu wa  miundombinu.
Kwa upande wake mratibu mkazi  umoja wa mataifa nchini Alvaro Rodriguez ameishukuru serikali ya tanzania kwa kukubali kuwapokea raia hao wa Burundi ambao wamekimbia machafuko katika nchi yao na kwamba jumuia ya kimataifa kwa kushirikiana na mashirika yanayotoa huduma kwa wakimbizi itaendelea kusaidia ili kuhakikisha wakimbizi na jamii ya watanzania inakuwa salama
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment