Image
Image

UN:Ipo haja mashirika ya ndani na nje kuwasaidia wakimbizi elfu hamsini wa Burundi Tanzania.

UMOJA wa mataifa (UN) umesema,kuna haja ya mashirika ya ndani na nje kujitolea kuwasaidia zaidi ya wakimbizi elfu hamsini wa Burundi waliokimbilia Tanzania kutokana na hali mbaya ya makazi,maradhi na maisha katika kambi ya nyarugusu wanakohifadhiwa kwa muda hivi sasa.
Mratibu mkazi wa umoja wa mataifa nchini ALVARO RODRIGUES amesema, kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi katika kambi ya nyarugusu, ambayo sasa ina wakimbizi karibu laki moja kufuatia wakimbizi karibu elfu hamsini toka burundi kupelekwa katika kambi hiyo, hali ya utoaji wa huduma za kijamii imekuwa ngumu na kwamba hatua ya serikali kutoa eneo la kujenga kambi mpya litasaidia kuepusha madhara katika kambi hiyo ambayo sasa ina wakimbizi toka burundi na kongo DRC.
mkuu wa kambi ya wakimbizi nyarugusu SOSPETER BOYO amesema kutokana na ujio huo, wamelazimika kufunga shule, na kutumia majengo ya shule na viwanja vya michezo kuwahifadhi jambo ambalo limeanza kuleta mgongano kati ya wakimbizi hao ambao wana tamaduni na mila tofauti.
kwa upande wake waziri wa mambo ya ndani mh mathias chikawe amesema tayari serikali imetenga eneo la migunga wilayani humo  kwa ajili ya kujenga kambi mpya ili kuwahamishia wakimbizi wa burundi  na kwamba serikali pamoja na mashirika ya kimataifa yamelazimika kuongeza huduma katika kipindi hiki ambacho mchakato wa kuwapa au kutowapa hadhi ya  ukimbizi ukiendelea kwa mujibu wa sheria.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment