Image
Image

Wazee waliokosa huduma ya choo kwa kujisaidi vichakani sasa wapata ahueni.


Baada ya wazee wanaoishi katika kituo cha makazi ya wazee wasiojiweza cha Kolandoto manispaa ya shinyanga kulalamika kwa muda mrefu kutokana na tatizo sugu la ukosefu wa choo na kulazimika kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo vichakani hatimaye tatizo hilo limepatiwa ufumbuzi kwa kujengewa choo na taasisi ya EASY FLEX.
Akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa choo hicho na kukabidhi msaada wa viti 30 na magodoro 60 kwa ajili ya malazi ya wazee hao vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 mratibu wa EASY FLEX Bi. Happyness Kihama amesema taasisi yake imeamua kuwajengea choo na kutoa msaada huo kutokana na kuguswa na matatizo yanayowakabili wazee hao kituoni hapo ikiwa pia ni kuwaepusha na magonjwa ya mlipuko kutokana na kujisaidia hovyo.
Akipokea msaada huo na jengo la choo chenye matundu manne kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa shinyanga Bw. Ally Rufunga mstahiki meya wa manispaa ya shinyanga Bw. Gullam Hafidh pamoja na kuishukuru taasisi hiyo ameitaka jamii ya watanzania kuwa na mwamko wa kuanza kuwasaidia wazee na watu wenye mahitaji maalum badala ya kusubiri misaada kutoka kwa wahisani wa nje ya nchi hali ambayo imekuwa ikidhalilisha utu wa mtanzania. 
Kwa upande wao mlezi msaidizi wa kituo hicho Bi. Evodia Ndaka  na mwenyekiti wa makazi hayo simon maganga  wameiomba serikali kuzifanyia ukarabati mkubwa nyumba za makazi hayo ya wazee kutokana na majengo yake kuchakaa hali inayowafanya waishi kwa wasiwasi mkubwa na kwamba wamekuwa  wakilazimika kuzihama wakati wa mvua inaponyesha kutokana na kuvuja huku nyingi kati ya hizo tayari sehemu za kuta zake zimebomoka.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment