Image
Image

Canavaro ahofia kuikosa Uganda wikiendi hii.


NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro' ameingia hofu ya kukosa mchezo wa marudiano wa michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani, kati ya Taifa Stars na Uganda 'The Cranes' utakaochezwa wikiendi hii.
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa mjini Zanzibar, Taifa Stars ilikubali kichapo cha mabao 3-0 hivyo timu hiyo ya Tanzania inayonolewa na Boniface Mkwassa, italazimika kushinda mabao 4-0 kwenye mchezo wa marudiano utakaofanyika nchini Uganda ili iweze kusonga mbele.
Canavaro ameingia hofu hiyo, baada ya kuumia wakati wa mchezo maalumu wa kuchangia kituo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino) kati ya Yanga dhidi ya SC Villa ya, iliyochezwa juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo timu hizo zilitoa suluhu.
Akizungumza mara baada ya mechi hiyo, Canavaro alisema kutokana na maumivu aliyonayo yanaweza kupunguza kasi ya kiuchezaji katika mechi hiyo dhidi ya Uganda.
Canavaro katika mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa na timu hizo kutoka suluhu, alipasuka paji la uso na kulazimika kushonwa nyuzi sita katika kidonda hicho.
"Nahofia kuzikosa mechi zilizopo mbele yetu kwa sasa kulingana na kuwa na maumivu katika paji la uso, najua umuhimu wa michezo iliyopo mbele yetu.
"Unajua nahitajika katika kikosi cha timu ya taifa na pia michezo mingine ya kujifua kwenye timu yangu, ambayo inatazamia kucheza katika michuano ya Kombe la Kagame," alisema.
Alisema jeraha alilolipata si zuri kwa kuwa alikuwa na mipango mingine ya kimaisha na familia yake, hivyo kuumia kwake kumekuja katika wakati mbaya kwake.
Katika mchezo huo uliochezwa juzi wachezaji wengi wapya wa Yanga walicheza katika malengo huku safu ya ulinzi ikijitahidi kuokoa mashambulizi ya kushtukiza ya washambuliaji wa SC Villa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment