Image
Image

Hongera Serikali kusikiliza wanahabari.

Tangazo la kuondolewa kwa muswada huo lilitolewa juzi bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya aliyesema uamuzi huo unalenga kuufanya uboreshwe na kupunguza madhara yanayoweza kutokea kwa jamii baadaye.
Juzi Serikali ilikubali kuundoa Muswada wa Sheria ya Upatikanaji Habari ya 2015 ili upelekwe kwa wadau kwa lengo la kuujadili na kukubaliana katika vipengele ambavyo wameviona vina matatizo.

Tangazo la kuondolewa kwa muswada huo lilitolewa juzi bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya aliyesema uamuzi huo unalenga kuufanya uboreshwe na kupunguza madhara yanayoweza kutokea kwa jamii baadaye.

Muswada huo, ambao ulikuwa unapingwa vikali na wanahabari na wadau, wakiongozwa na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Baraza la Habari (MCT) na Jukwaa la Wahariri (TEF), ulichapishwa Februari 20, 2015 na kusomwa kwa mara ya kwanza kwenye vikao vya Bunge vya Machi hadi Aprili.

Ulitakiwa usomwe kwenye Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma, lakini wanahabari waliongeza sauti ya kilio chao na kusababisha Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii kujadili kwa kina na kufikia uamuzi.

Akisoma taarifa ya Serikali, Profesa Mwandosya alisema baada ya kupokea maoni ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Serikali imetafakari na kuafiki kuwa muswada huo uendelee kufanyiwa kazi hadi hapo kazi hiyo itakapokuwa imekamilika ipasavyo.

Alisema matarajio ya Serikali ni kwamba muswada huo utasomwa kwa mara ya pili na ya tatu kwenye Bunge la Kumi na Moja ambalo litapatikana baada ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Hizi ni habari njema kwa waandishi wa habari na wadau wote wa tasnia ya habari kwamba hatimaye Serikali imesikia kilio chao na kuamua hatua zinazotakiwa za kuupitisha muswada huo katika hatua mbalimbali, zifanyike ili baadaye muswada uende bungeni ukiwa na ridhaa ya pande zote.

Tunapenda kuipongeza Serikali kwa uamuzi huo wa busara wa kusikiliza kilio cha wanahabari, ambao hadi sasa wanafanya kazi kwenye mazingira magumu kutokana na kuwapo kwa sheria za kibabe ambazo nyakati fulani hutumiwa vibaya na kuwaumiza.

Huu ndiyo ungekuwa motto wa utendaji kazi wa Serikali wa kuhakikisha inashirikisha wadau katika masuala muhimu yanayowahusu watu wa sekta husika kabla ya kufanya uamuzi.

Dhana ya ushirikishwaji ndiyo inayotawala katika ulimwengu wa kisasa ambao umejaa watu waliosoma, waliopevuka, weledi na wenye uwezo wa kuchambua mambo. Katika dunia ya namna hiyo ni vigumu kuwaburuza watu katika kufanya uamuzi kwa kuwa utakabiliwa na upinzani mkubwa.

Hali kadhalika, dhana ya ushirikishwaji inaandaa mazingira ya kuiwezesha sheria inayoundwa kutekelezeka kwa kuwa inakuwa imepata ridhaa ya pande zote ambazo zinakuwa zimeshiriki kikamilifu tangu hatua za awali hadi mwisho.

Tunapenda kuipongeza Serikali kwa uamuzi huo na tunaamini kuwa itaendelea kusikiliza wadau wa sekta mbalimbali kila inapotaka kufanya uamuzi ambazo unawagusa wahusika.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment