Image
Image

KHUMLO anashikiliwa na serikali ya India kwa kuhusika na mauaji ya wanajeshi 20.


Serikali ya India imesema imemtia mbaroni kiongozi wa waasi, KHUMLO ABI ANAL kwa kuhusika na mauaji ya  wanajeshi 20 katika shambulio la kushitukiza  kwenye msafara wa wanajeshi hao Kaskazini-Mashariki mwa India.

ANAL ni kiongozi wa  kikundi kinachotaka kujitenga cha National Socialist Council of Nagaland .

Shambulio hilo limetokea mwezi uliopita jirani na mpaka wa  Myanmar   katika Jimbo la   Manipur  na kutokana na shambulio hilo Jeshi la India  limelipiza kisasi kwa kushambulia kambi a waasi ndani ya Myanmar siku kadhaa baada ya shambulio hilo dhidi ya msafara wa jeshi.

Jeshi la  India  limesema liliteketeza kambili mbili za waasi  ndani ya  Myanmar  na kurejea salama, madai ambayo yamekanushwa na  Myanmar.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment