Image
Image

Watu 30 wafaa baada ya ndege ya mizigo ya jeshi kuanguka kwenye makazi ya watu Mji wa Medan.


Watu  30 wamekufa  na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya ndege ya mizigo ya jeshi la Indonesia kuanguka kwenye makazi ya watu  katika Mji wa Medan nchini humo.

Televisheni ya  Indonesia  imeripoti kuwa ndege hiyo imeangukia  kwenye nyumba mbili na gari  na kisha kuwaka moto.

Msemaji wa Jeshi la Indonesia,FUAD BASYA  amewaambia Waandishi wa Habari kuwa ndege hiyo imeanguka muda mfupi baada ya kuruka na ilikuwa na wafanyakazi 12.

Msako mkubwa unaendeshwa kwenye eneo  ndege hiyo ilipoanguka ambayo limekumbwa na miali ya moto na moshi mzito.

Waandishi wa Habari wanasema hii ni maraya pili katika kipindi cha miaka kumi, ndege kuanguka kwenye vitongoji vya Mji wa Medan.

Septemb a  2005, ndege aina ya  Boeing 737  ilianguka kwenye  makazi ya watu muda mfupi baada ya kuruka  kutoka Uwanja wa Ndege wa Polonia  na kusababisha vifo vya watu  143 ,wakiwemo 30 waliokuwa ardhini.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment