Image
Image

Ushawahi kufikiria kuwa uyoga una tibu unene,huu ndio ukweli soma hapa.

Uyoga ni moja ya mboga ambayo imekuwa ikiliwa na baadhi ya watu hapa nchini, lakini je, umewahi kuwaza kuwa mboga hiyo inaweza kuwa dawa? Na kama dawa unadhani ni dawa ya nini hasa?
Majibu ya maswali hayo yanapatikana kutoka katika hii stori kutoka nchini Taiwan, ambapo wao uyoga kwao hutumika kama dawa ya kupunguza unene.
Kwa miaka sasa uyoga umekuwa ukitumika nchini humo kama dawa ya kupunguza unene katika wanyama, hayo yamesemwa na watafiti nchini Taiwan.
Utafiti huo, uliochapishwa katika jarida la mawasiliano ya mazingira umebainisha kuwa madini ya 'Ganoderma Lucidum' yaliyomo ndani ya uyoga, hupunguza taratibu uwezo wa mtu kuwa na uzito mkubwa kwa kutatiza bakteria ndani ya utumbo.
Imeelezwa kuwa madini hayo ya 'Ganoderma Lucidum' yaliyomo ndani ya uyoga, hupunguza taratibu uwezo wa mtu kupata uzani
Wataalam wanasema kuwa sayansi hiyo ni nzuri, lakini kuweka maji yanayotokana na uyoga kwenye mikebe ya cola hakutawasaidia watu kupunguza uzani.
Mbali na hayo Watafiti katika chuo Kikuu cha Chang Gung wamesema kuwa madini hayo ya G. lucidum yameuwa yakiuzwa tangu jadi kama kichocheo cha "kiafya na kurefusha maisha"
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment