Image
Image

Vikosi vya Usalama nchini Chad vimewatia mbaroni watu 60 waliohusika na mashambulio mawili ya mabomu ya kujitoa muhanga Mji mkuu wa Chad, N'Djamena.


Vikosi vya Usalama nchini Chad vimewatia mbaroni watu 60 wanaotuhumiwa kuwa ni wanamgambo waliohusika na mashambulio mawili ya mabomu ya kujitoa muhanga kwenye Mji mkuu wa Chad, N'Djamena tarehe 15 mwezi huu.

Milipuko miwili  ya mabomu ya kujitoa muhanga  kwenye ofisi  mbili za Polisi Mjini N'Djamena, ambayo inaonekana kuratibiwa na wapiganaji wanne wa kikundi cha Kiislam cha Boko Haram na kusababisha vifo vyawatu 34 wakiwemo watuhumiwa wanne  wa Boko Haram na kuwajeruhi wengine kadhaa.

Mwendesha Mashitaka mkuu nchini Chad, Bwana  ALGHASSIM KHAMIS amesema katika operesheni hiyo mtandao wa ugaidi wa Boko Haram umeteketezwa.

Amesema wapiganaji wa Boko Haram waliotiwa mbaroni wanatoka mataifa ya Chad, Cameroon, Mali  na Nigeria.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment