Image
Image

Wanajeshi 11 wa Afghanistan wameuawa katika shambulio la kushitukiza.


Wanajeshi  11 wa Afghanistan wameuawa katika shambulio la kushitukiza lililofanywa na wapiganaji wa Taliban, Magharibi mwa nchi hiyo.

Msemaji wa gavana wa Jimbo la Herat, Bwana  EHSANULLAH  HAYAT, amesema wapiganaji  hao wa Taliban  waliushambulia msafara wa wanajeshi hao katika Wilaya ya Karukh  jana usiku na kusababisha vidfo vya wanajeshi hao 11.

Amesema wanajeshi hao walikuwa wakisafiri kwenye magari madogo ya mizigo Pick-Up.

Naye Msemaji wa Jeshi  Magharibi mwa Afghanistan Bwana NAJIBULLAH NAJIBI, amethibitisha kutokea kwa shambulio hilo na kuongeza wanajeshi wanne pia wamejeruhiwa katika tukio hilo.

Wanajeshi wa Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi  - NATO- wakiongozwa na Marekani waliondoka Afghanistan Desemba mwaka jana na kuwaacha maafisa wachache kwa ajili ya kutoa mafunzo na kuvisaidia vikosi vya usalama.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment