Image
Image

Wapya Yanga wamkuna kocha.

KOCHA wa Yanga, Hans van der Pluijm amevutiwa na viwango vya wachezaji wake wapya katika kikosi hicho kwa kile alichokisema kuwa wote wamefanya vizuri katika mchezo wa juzi.
Katika mchezo huo wa kirafiki uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa kati ya Yanga dhidi ya Sports Club Villa ya Uganda, timu hizo zilitoka suluhu.
Wachezaji wapya wa Yanga waliocheza kikosi cha kwanza ni Deus Kaseke, Malimi Busungu na Godfrey Mwashiuya, ambao kwa mujibu wa Pluijm, walicheza vizuri kwa kujituma.
“Wachezaji wote wamejitahidi wamecheza vizuri, wameshirikiana vizuri katika kikosi hicho,” alisema. Licha ya kuwa mchezo huo ulikuwa ni kwa ajili ya kuwachangia walemavu wa ngozi (maalbino) ulitumika pia kuwapima wachezaji hao wapya kwa kuwaonesha mashabiki viwango vyao.
Wachezaji hao kila walipokuwa wakigusa mpira na kucheza vizuri walikuwa wakipigiwa makofi na mashabiki wa klabu hiyo waliohudhuria kwa wingi huku wengine wakionekana kuvutiwa na viwango vyao kutokana sifa walizokuwa wakizitoa wakati mechi inaendelea.
Pluijm alizungumzia pia kuhusu kiwango cha timu na kusema licha ya kucheza vizuri walitamani kupata ushindi. “Kikosi kilicheza vizuri, tulitengeneza nafasi za kufunga lakini bahati haikuwa ya kwetu, wenzetu walianza vizuri lakini baadaye wakajikuta wanacheza kwa kuzuia,” alisema.
Alisema mchezo huo umempa nafasi ya kujua baadhi ya mapungufu, hivyo atayafanyia kazi na kujipanga kwa ajili ya michezo mingine ijayo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment