Image
Image

Mbilinyi awataka watanzania kutumia uchaguzi mkuu ujao kubadili mfumo wa uongozi.



Ikiwa ni siku chache tu baada ya Rais Kikwete kulivunja bunge la 10 mjini Dodoma hatimaye watanzania wameaswa kutumia uchaguzi mkuu ujao kuweza kubadili mfumo wa uongozi ili waweze kujiletea maendeleo badala ya kubadilisha watu katika nafasi za maamuzi hali ambayo inadaiwa kuendelea kudidimiza uchumi wa nchi na maisha ya mwananchi mmoja mmoja.
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa mbeya mjini,Joseph Mbilinyi jijini mbeya wakati alipo wasili na kupata mapokezi makubwa na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua awatumikie kwa miaka mitano,amesema kuwa tatizo la uongozi wa Tanzania sio watu bali ni mfumo unaotumika kuendesha taifa.
Baadhi ya viongozi wa chadema wamewataka wananchi kukiamini chama hicho kwa kuwa ndicho pekee chenye nia na dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko ya uongozi nchini.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha Demokrasia wilaya ya mbeya mjini,David Mwambigija amesema kuwa jiji la mbeya linakusudia kuanza mabadiliko ya mfumo wa kiuongozi kwa chadema kuongoza halmashauri ya jiji la mbeya, hivyo akawataka wananchi kuwachagua madiwani wengi wa chadema ili kutimiza azma hiyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment