Image
Image

Jeshi la Nigeria laokoa watu 71 katika operesheni iliyotekelezwa dhidi ya Boko Haram.


Jeshi la Nigeria limeripotiwa kutekeleza operesheni katika vijiji viwili vilivyokuwa vimetekwa na Boko Haram katika mkoa wa Konduga.
Jeshi hilo pia lilifanikiwa kuokoa watu 71 waliokuwa wamechukuliwa mateka na wanamgambo wa kundi la Boko Haram.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na msemaji wa jeshi, miongoni mwa mateka hao waliookolewa kutoka mikononi mwa Boko Haram mlikuwa ni watoto 25, wanawake 29 na wazee 5.
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba wanamgambo wengi wa kundi la Boko Haram pia waliuawa, huku gari moja aina ya Jeep pamoja na lori likikamatwa wakati wa operesheni hiyo.
Kambi mbili zinazoshukiwa kutumika kama ngome kuu za wanamgambo wa Boko Haram pia ziliharibiwa katika maeneo ya Kashimbiri na Warmure.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment