Image
Image

LUBUVA-TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutoa fomu za urais,Ubunge pamoja na Udiwani kesho.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa yaUchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu,Damian Lubuva (katikati) akizungumza na waandishi habari juujuu ya maendeleo mbalimbali katika kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika leo MakaoMakuu ya NEC jijini Dar es Salaam,Kulia Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dares Salaam,Kamishina Suleiman Kova na Kushoto ni Mkuu wa Idara ya UendeshajiUchaguzi,Clothilde Komba.

 Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumuya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akizungumza na waandishi habari juujuu  jeshi la polisi lilivyojipangakatika suala la ulinzi kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika leo Makao Makuu yaNEC jijini Dar es Salaam.

Waandishi wa habari wakifatilia wataarifa ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Damian Lubuvaleo Makao Makuu ya NEC jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka waGlobu ya Jamii).\
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kuanza kutoa fomu ya urais ,Ubungepamoja na Udiwani kesho na kumalizika kwa zoezi la utoaji fomu hizo ni Agasti21 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habarileo jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,JajiMstaafu,Damian Lubuva  amesema wakati wauchukuaji wa fomu ya urais itatolewa bure lakini wakati wa kurudisha anatakiwakuweka dhamana ya Sh.milioni Moja na wadhamini wadhamini 200 katika kila mkoana kuwepo kwa mikoa miwili Zanzibar.
Lubuva a amesema kuwa wakati wakuchukua fomu viongozi wa vyama vya kisiasa wanatakiwa kuchukua fomu nakurudisha bila kuwa na kundi kubwa ambalo linaweza kusimamisha shughuli za watuwengine.
Amesema kwa fomu za ubunge nish.50,000  na udiwani sh.5000 ambapowanatakiwa kuchukulia katika ofisi za wilaya na uchukuaji huo lazima uwe wakistaarabu katika kuweza watu wengine waendelee na shughuli zao.
Lubuva amesema kuwa  wanasiasa wanatakiwa  na lugha za kistaarabu katika mikutano yao
katika kujenga demokrasia iliyo ya ukweli.
Hata hivyo amesema kuna baadhi yavijana wanauza kadi za tume ya taifa ya uchaguzi na kutaka vyombo vya usalamakuchunguza pamoja na kuwachukulia hatua watu wanaouza kadi hizo.
Kamanda wa Polis wa Kanda Maalum yaDar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova amesema kuwa uchaguzi unaendana  na usalama hivyo jeshi limejipanga katikaulinzi katika kipindi hiki.
Kova amesema kuwa Jeshi litaendeleakushirikiana na viongozi wa siasa katika kuleta amani katika kipindi chauchaguzi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment