Image
Image

Mukulu muasi wa ADF apelekwa Uganda.

Kiongozi wa kundi la waasi wa Uganda la Allied Democratic Forces-ADFJamil Mukulu amekabidhiwa kwa serikali ya Uganda kutoka Tanzania.
Alikamatwa akiwa akijaribu kumpatia mtoto wake kibali cha kusafiria cha Tanzania. Kundi la ADF limekuwa likipigana dhidi ya utawala wa sasa wa Kampala kwa miaka takriban 20 na kutumia mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo kama maficho na kuipelekea Uganda kuigia kijeshi nchini humo ikimsaka.
Mukulu ameonyeshwa kwa waandishi habari nchini Uganda na Mkuu wa polisi Generali kale kaihura ambae ameelezea kufurahishwa kwao na kukamatwa kwa Mukulu.
Serikali ya Uganda imesema kuwa Jamil Mukulu ambaye wamekuwa wakimsaka kwa zaidi ya miaka 20 kwa sasa wanatarajia kumfikisha katika mkondo wa sheria.
General Kale Kaihura ametoa onyo kwa baadhi ya makundi ya waasi ambayo yamekuwa yakiua raia na kisha kujificha nchi jirani,kwamba watabainika tu na kufikishwa katika mkondo wa sheria.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment