Image
Image

TUNDULISU:Hatukudanganya kumuweka Mh.Lowassa kwenye Orodha ya mafisadi hata kidogo.


Wakati chama cha Demokrasia na Maendeleo chadema kikimtambulisha rasmi aliyekuwa Waziri mkuu mstaafu kupitia chama cha mapinduzi CCM,Edward Lowassa  kuwa mwanachama mpya wa chama hicho cha demokrasia na maendeleo CHADEMA,Huku kukiwa na Minong’ono ya chini chini kuwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA  ambao hawakuwepo wakati wa mapokezi na utambulisho wa mwanachama mpya ndani ya chama hicho walikasirika na kususia sherehe hiyo hatimaye Tundu lissu ameweka bayana kuhusu suala hili.
Lissu-amesema kuwa kutokuwepo katika mapokezi ya Waziri mkuu huyo Edward Lowassa ni kwamba kulikuwa na majukumu mengine ambayo alikuwa akiyashughulikia lakini alikuwa mwenye kufuatilia mapokezi namna yalivyokuwa yakiendelea na kusema ni mapokezi ambayo yalifana sana na yalijenga historia ya aina yake kwa taifa letu hili la Tanzania.
Tangu tumepata uhuru kutoka kwa waingereza na hasa tangu tumeingia katika mfumo wa vyama vingi haijawahi kutokea katika nchi hii mtu wa aina ya Edward Lowassa akaondoka kwenye chama tawala akaenda kwenye Upinzani haijawahi kutokea unapoona yanatokea sasahivi yanakuambia kwamba hiki sikipindi cha kawaida ni kipindi cha mabadiliko.Amesema Lissu.
Kuhusu Mh.Lowassa kuitwa fisadi na wabunge wa upinzani na hivyo kuonekana kama kusafishwa ndani ya chadema ,Lissu anasema kuwa kuhusu hilo yeye ndiye alikuwa mwandishi mkuu wa kuandika orodha ya Mafisadi kwa kushirikiana na Dkt.Slaa,jambo ambalo anakiri kuwa hawakudanganya hata kidogo alisema kuwa Lowassa kwa ushiriki wake katika kashfa ya RICHMOND anafaa kuwa kwenye Orodha ya Mafisadi.
Ukisema haikuwa RICHMOND hapana ilikuwepo ilikuwa kashfa kubwa waziri mkuu alilazimishwa kujiuzulu lakini tunafahamu vilevile kwamba haiwezekani kitu kikubwa kama RICHMOND kikatokea kikafanywa na mtu mmoja waziri mkuu haiwezekanii washiriki wengine ni kinananiii???? Majibu ametupa jana. Amesema Lissu.
Haya ndio Majibu ya TUNDU LISSU kuhusu kutokuhudhuria katika hafla ya kumpokea Mh.Lowassa ndani ya CHADEMA,anaongea hapa#Bofya Kusikia,na kwa Taarifa Endelea kufuatilia Taarifa zetu kumbuka pia ku Like Page yetu hapo juu>>
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment