Image
Image

UDM-Yamtunuku Museveni Shahada ya Udaktari yaheshima.


Chuo kikuu cha Dar es Salaam kimemtunuku shahada ya udaktari wa heshima rais ya Uganda Daktari Yoweri Kagutta Museveni kutokana na mchango wake katika kuimarisha umoja wa nchi za Afrika.

Akizungumza  katika hafla fupi ya kutunuku shahada hiyo,makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es salaam Profesa  Rwekaza Mukandara licha ya kupongeza jitihada za kiongozi huyo katika kuziunganisha nchi za Afrika amepongeza ushirikiano wake na chuo kikuu cha Dar es Salaam, na kusisitiza chuo hicho kinakabiliwa na tatizo la rasimali ili kuweza kukamilisha ujenzi wa miradi ya chuo ikiwemo mambo mbalimbali.

Rais wa Uganda Dkt.Museveni Amesema amepongeza jitihada zinazofanywa na chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa kuandaa viongozi bora toka uongozi wa baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere, hususani katika masomo ya sayansi ya siasa,sayansi ya jamii na kusistiza moja ya changamoto inazozikabili nchi za Afrika  na kugundua matatizo yanayozikabili jamii na uwezo mdogo wa kufuatilia.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment