Image
Image

Viongozi wa dini waaswa kuhubiri amani kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu nchini Tanzania.



Viongozi wa dini nchini wameaswa kuhubiri amani kwa waumini wao na kuepuka uchochezi unaofanywa na baadhi ya wanasiasa hasa katika kipindi hiki taifa linapoelekea katika uchaguzi mkuu hali itakayosaidia kutofanyika vitendo vinavyoweza kuvuruga amani na kuligharimu taifa kwa kumwaga damu za watu wasio na hatia.

Akizungumza katika mkutano maalum wa kuliombea taifa amani, ulioandaliwa na jumuia ya waislam ya wa Ahamadia Kanda ya Ziwa Victoria, kiongozi mkuu wa wa jumuia hiyo, Sheikh TAHIR MAHMOOD CHAUDHRY amesema inashangaza kuona vitendo vinavyovunja amani vinaendelea kushamiri kwa kasi duniani hivyo viongozi wa dini wasipotilia mkazo mafundisho na maonyo kwa waumini wao kuna hatari ya kuzuka kwa vita kuu ya tatu ya dunia.

Wakizungumzia hali hiyo, baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wa amani wamewataka viongozi wa dini ya Kiislam kuwaelimisha Watanzania juu ya neno Jihad,  kwa kuwa kwa kumekuwepo na mkanganyiko katika tafsiri yake na kwa wakati mwingine kutishia kuvurugika kwa amani.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,  ALLY NASORO RUFUNGA amesema amani ni kiungo muhimu kinachounganisha viumbe vyote duniani huku akitoa wito kwa viongozi wa dini ,serikali na vyama vya siasa kuendelea kuhubiri amani.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment