Mara
baada ya kikao cha bunge kuanza spika wa bunge alinza kwa kuwakumbusha wabunge
namna ya kufuata kanuni hasa pale wanapotaka kuondoa muswada wowote na
alipomaliza Mh.Wenje akaomba muongozo wa spika ambapo alitaka kusitishwa kwa
miswada hiyo na hapo ndipo vurugu zikaanza tena lakini safari hii spika
hakuahirisha bunge badala yake akawatoa nje na hapa hali ikawa hivi.
Nje
ya ukumbi wa bunge wabunge hao waliotolewa nje wakazungumza na waandishi wa
habari wakaelezea kitendo cha wao kutolewa nje pamoja na sababu za wao kuikataa
miswada hiyo kuletwa yote pamoja na kwa hati ya dharura.
Hata
hivyo baada ya vurugu zote kuisha miswada yote mitatu ambayo ni sheria ya
petroli, sheria ya usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi pamoja na sheria ya
uwazi na uwajibikaji katika tasnia ya uchimbaji Tanzania ambapo akiwasilisha
muswada wa petroli bungeni mjini dodoma waziri wa nishati na madini Mh.Simba Chawene
amesema mswada huo utajenga mfumo imara wa kusimamia sekta ya mafuta na gesi.
Wenyeviti
wa kamati hizo nao wakawasilisha maoni na ushauri wa kamati zao ambapo
mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini Mh. Richard Ndassa akisoma mani ya
kamati amesema kamati imekubalina na serikali kuhusu mamlaka aliyopewa waziri
pamoja na maoni ya wadau kuhusu kumuongezea waziri mamlaka kisheria kuingia
mikataba mikubwa ya miradi ya gesi asilia pasipo kuingilia au kuwa na mamlaka
sawa na TPDC.>>Bonyeza
SHARE Hapo juu uwezavyo ili washkaji zako wasipitwe na Stori kama Hizi
na Tunapokea matangazo maelekezo hapo kwenye ukurasa wetu yana jieleza
kuwa wa kwanza kutangaza nasi.
0 comments:
Post a Comment