Image
Image

DKT.Slaa aitaka serikali kuondoa mivutano na wananchi wake inayo pelekea uvunjifu wa amani.


Katibu mkuu wa Chama cha demokrasia na maendeleo chadema Dk. Wilbroad Slaa amesema kuwa njia pekee ya serikali kuondoa  mivutano na malumbano ya mara kwa mara kwa wananchi wake ni kufanya maamuzi ambayo yanatoa haki  kwa pande zote na kuhakisha kuwa inatafuta ufumbuzi wa kina wa migongano inayotokea na kusababisha amani kuvunjika.

Dk.Slaa ametoa kauli hiyo  wakati akizungumza  katika kongamano la  la kutafakari na wazee kuhusu uchaguzi  mkuu wa mwaka huu ambapo  amesema sasa umefika wakati wa kila mzee kutambua kuwa sasa ni muda  wa mabadiliko.

Awali  akitoa salamu zake Mh.Mabere Marando na ambaye ni mwenyekiti wa kanda ya Pwani amewaomba wazee kuhamasisha watu wajitokeza kujiandikisha ili waweze kupata nafasi nzuri ya kupiga kura ,kura amabyo italeta mabadiliko  katika nchi.

Kwaupande wake Mh.Hashim Juma  mwenyekiti wa baraza la  wazee wa chama hicho amesema kwa kipindi kirefu wazee wamesahaulika nchini  na hivyo umefika muda  wa kubadilisha mfumo ili waweze kupata haki zao.




Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment